1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUjerumani

Chama cha Verdi chaitisha mgomo wa siku tatu wa Luftansa

27 Februari 2024

Chama cha wafanyakazi wa huduma nchini Ujerumani, Verdi kimeitisha mgomo wa siku tatu wa wafanyakazi wa shirika la ndege la Luftasa kuanzia Jumatano. Ni baada ya mazungumzo juu ya nyongeza ya mishahara kushindikana.

https://p.dw.com/p/4cxes
Onyo la mgomo wa wafanyakazi wa Lufthansa
Mgomo wa siku tatu wa Lufthansa unawahusu wafanyakazi wa ufundi na vitengo vingine.Picha: Boris Roessler/dpa/picture alliance

Chama cha wafanyakazi cha Ujerumani Verdi kimetoa wito wa kufanyika kwa mgomo wa siku tatu nchini kote wa wafanyikazi wa Lufthansa kuanzia Jumatano huku mpambano wa mishahara na shirika hilo linalopeperusha bendera ya Ujerumani ukiendelea. Safari za ndege za abiria hazitaathiriwa, chama hicho kimesema.

Kusitishwa kwa kazi katika mzozo wa majadiliano ya pamoja kunaathiri wafanyakazi na wafunzwa katika vitengo vya Lufthansa Technik, Mafunzo ya Usafiri wa Anga vya Lufthansa na Mafunzo ya Kiufundi ya Lufthansa, ilisema Verdi Jumanne jioni.

Wafanyakazi wa Lufthansa Technik Logistik na Lufthansa Technik Logistik Services watajiunga na mgomo huo kwa nyakati tofauti kulingana na eneo, na hivyo kupunguza usumbufu.

Mgomo wa wafanyakazi wa Lufthansa
Tayari Verdi imeitisha migomo mwili ya wafanyakazi wa Lufthunsa tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2024.Picha: Boris Roessler/dpa/picture alliance

Lufthansa ilisema inachukulia kwamba mgomo wa onyo wa siku tatu uliopangwa kwa wafanyakazi wa kiufundi "hautaleta athari kubwa kwenye ratiba ya safari za ndege za Lufthansa" siku ya Jumatano.

Shirika hilo la ndege liliwashauri abiria kuangalia hali ya safari zao kwenye lufthansa.com au katika app ya Lufthansa. Shirika hilo lilisema kwa sasa linaangalia athari za mgomo huo kwa operesheni za Alhamisi na Ijumaa.

Soma pia: Maafisa usalama wa viwanja vya ndege waitisha mgomo Ujerumani

Chama cha Verdi tayari kimefanya migomo miwili ya siku moja mwezi huu. Mgomo wa hivi karibuni zaidi ilikuwa ya wafanyakazi wa ufundi, vifaa na kaunta ulikuwa Februari 20, wakati Lufthansa ilipolazimika kuahirisha asilimia 90 ya safari zake za ndege.

Verdi yasema ofa ya Lufthansa haitoshi

Migomo hiyo ililemaza shughuli za Lufthansa katika vituo vyake vya Munich na Frankfurt, lakini safari za ndege pia zilikatishwa katika viwanja vingine vingi vya ndege.

Baada ya duru za awali za mazungumzo, Verdi hivi karibuni ilikataa ofa nyingine isiyotosha kutoka kwa Lufthansa kufuatia mazungumzo ya siku mbili ya mshahara.

Lufthansa wakati huo ilisema ilikuwa imepiga "hatua kubwa kuelekea Verdi" na ikawasilisha "ofa mpya iliyoboreshwa."

Mgomo wa madereva reli.

Miongoni mwa maboresho yaliwekwa mezani ni ongezeko la mishahara la asilimia 4 kuanzia mapema Machi na bonasi ya fidia ya mfumuko wa bei ya  euro 3,000 ambayo ilipaswa kulipwa mapema kuliko ilivyopangwa awali.

Verdi inasema ofa ya Lufthansa bado haitoshi. Duru inayofuata ya mazungumzo imepangwa Machi 13-14.

Chanzo: DPAE