1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUjerumani

Wafanyakazi wa Lufthansa waanza mgomo

Bruce Amani
20 Februari 2024

Mgomo wa pili wa wafanyakazi wa Lufthansa umeanza jana, huku shirika hilo la ndege la Ujerumani likitarajia mamia ya safari kufutwa na zaidi ya abiria 100,000 kuathiriwa.

https://p.dw.com/p/4cb1O
Chama cha wafanyakazi verdi kinadai nyongeza ya mshahara
Abiria 100,000 wanatarajiwa kuathirika na mgomo wa shirika la LufthansaPicha: Michael Probst/AP/picture alliance

Kampuni hiyo tayari imefuta safari kadhaa za kuunganishwa katika uwanja wake mkuu mjini Frankfurt na ni safari chache tu za kimataifa zilizopangwa kuendelea.

Chama cha wafanyakazi Ujerumani verdi kimesema wafanyakazi wa idara za teknolojia, vifaa na usafirishaji, mizigo na habari na mawasiliano wanagoma. Wahudumu wa Lufthansa katika viwanja vya Frankfurt, Munich, Hamburg, Berlin, Dusseldorft, Cologne/Bonn na Stuttgart pia wanagoma. Mgomo huo utamalizika kesho Jumatano. 

Lufthansa inasema wahudumu wake 20,000 wanahusika katika mgomo huo. Chama cha verdi kinasema makubaliano hayajafikiwa katika duru ya tatu ya mazungumzo, ambapo ofa ya Lufthansa kwa wafanyakazi wa viwanja viwanja ndege ikikataliwa na wengi wa wafanyakazi wake. Verdi inadai nyongeza ya asilimia 12.5 ya mshahara wakati Lufthansa inapendekeza nyongeza ya asilimia 10 katika miezi 12