1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Hamas cha Palastina kimesema kitasusia chaguzi za urais na bunge zitakazoitishwa na Rais Mahmud Abbas.

17 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CBHu

Gaza:

Chama cha Hamas chenye siasa kali za Kiislamu kitasusia chaguzi za urais na bunge huko Palastina. Waziri mkuu, Ismail Haniya, alilielezea tangazo la Rais Mahmud Abbas la kuitisha uchaguzi wa mapema kuwa ni la uasi na akambebesha dhamana ya kuzidi mapambano ya madaraka baina ya Wapalastina wenyewe kwa wenyewe. Chama cha Hamas, ambacho kimekuwa kikiendesha serekali chini ya mwaka mmoja sasa, kimesema hatua yeyote ya kuitisha uchaguzi wa mapema itaamanisha mapinduzi. Rais Abbas hajataja tarehe ya kufanywa chaguzi hizo, na akasema bado yuko tayari kufanya mazungumzo na Chama cha Hamas juu ya kuundwa serekali ya Umoja wa Taifa.

Kumeripotiwa kusikika milio ya risasi katika makao ya rais na katika si chini ya wizara mbili zinazoendeshwa na Chama cha Hamas. Zaidi ya hayo ni kwamba mlolongo wa magari uliomuungoza waziri wa mambo ya kigeni Mahmud al-Zahar ulifyetuliwa risasi. Masaa machache kabla, wapiganaji wa Chama cha Hamas waliishambulia kambi ya mafunzo ya walinzi wa Rais Abbas. Mwanajeshi mmoja aliuwawa na watatu wengine walijeruhiwa.