1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDU yafutilia mbali ushirikiano wowote na AfD ama Die Linke

21 Februari 2026

Kiongozi wa kundi la wabunge wa kihafidhina Ujerumani, Jens Spahn, amefutilia mbali uwezekano wowote wa ushirikiano na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD na kile Chama cha Mrengo wa Kushoto, Die Linke.

https://p.dw.com/p/59BzA
Ujerumani Stuttgart 2026 | mkutano wa CDU
Kiongozi wa kundi la wabunge wa kihafidhina Ujerumani, Jens Spahn akihutubia mkutano mkuu wa CDU mjini Stuggart mnamo Februari 21, 2026Picha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa chama tawala cha Christian Democratic Union (CDU) mjini Stuttgart, Spahn alikishutumu chama hicho chenye siasa kali za mrengo wa kushoto kwa chuki dhidi ya Wayahudi miongoni mwa wanachama wake wakuu na kuendelea kuwa na ujamaa katika mipango yake.

Pia alikikososa vikali chama cha AfD kwa kuwa karibu na Urusi. Amesema chama hicho kimepoteza mwelekeo kabisa .

Alimkosoa moja kwa moja kiongozi wa kundi la wabunge wa mrengo wa kushoto Heidi Reichinnek, na kumlinganisha na kiongozi wa zamani wakikomunisti Ujerumani Mashariki, Erich Honecker.

Akizungumzia kashfa ya hivi majuzi iliyohusisha wabunge wa AfD kuajiri wanafamilia wa kila mmoja wao kama wasaidizi, Spahn alisema huo ni usaliti wa taifa na walipa kodi.