CAIRO:Kituo cha Tv kinachofagilia mashambulio ya wasunni Iraq chafungwa,Misri | Habari za Ulimwengu | DW | 27.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO:Kituo cha Tv kinachofagilia mashambulio ya wasunni Iraq chafungwa,Misri

Misri imesimamisha kurusha matangazo ya kituo cha binafsi cha televisheni cha Iraq ambacho kinasifu uasi unaotekelezwa na wasunni nchini Iraq.

Marekani iliitaka binfasi Misri kusimamisha urushaji wa matangazo ya kituo cha al Zawraa ambacho kinapeperusha matangazo yake kupitia mitambo ya setiliti ya kituo cha televisheni ya serikali ya Misri.

Kituo hicho cha Al- Zawraa kinaendesha shughuli zake kutoka mahapa pasipojulikana na mmiliki wa kituo hicho alikuwa mbunge nchini Iraq ambaye kwa sasa anaishi nchini Syria.

Hata hivyo mmiliki wa kituo cha al Zawraa Mishan al Jaburi ameishutumu Misri kwa kutii shinikizo za Marekani za kutaka isimamishe matangazo ya kituo hicho.

Al Zawraa kilikuwa kinaonyesha picha za mashambulio yanayofanywa na wapiganaji wa kisunni dhidi ya vikosi vya Marekani na Iraq.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com