1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Bunge: Nyaraka za siri za Epstein zifichuliwe Marekani

19 Novemba 2025

Bunge la Marekani limepitisha muswada ambao utaweza kuilazimisha Wizara ya Sheria kufichua nyaraka zote za siri zinazohusiana na kashfa ya ngono ya mfanyabiashara Jeffrey Epstein.

https://p.dw.com/p/53r8v
Picha ya Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Jeffrey Epstein
Picha ya Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Jeffrey Epstein, anayeshukiwa kuwa walikuwa na uhusiano wa karibu.Picha: Phil Noble/REUTERS

Baraza la Wawakilishi liliidhinisha hapo jana muswada huo kwa kura 427 zilizounga mkono na moja tu ikipinga. Muswada huo sasa unasubiri kuidhinishwa na Rais Donald Trump ambaye pia inashukiwa kuwa alikuwa na uhusiano na Epstein, jambo ambalo Trump amelinakusha.

"Chochote kinachohusiana na nyaraka hizo za siri, sina uhusiano wowote na Jeffrey Epstein. Nilimfukuza kutoka klabu yangu miaka mingi iliyopita, kwa sababu nilidhani alikuwa mgonjwa na mpotovu. Na nadhani nilikuwa sahihi."

Jeffrey Epstein alikuwa mfanyabiashara tajiri wa Marekani na msimamizi wa mali za mabilionea wengi na rafiki wa watu mashuhuri akiwemo Trump. Alipatikana na hatia ya uhalifu wa kingono na kisha kufungwa jela akisubiri kusikilizwa kwa kesi iliyomkabili ya kusafirisha wasichana wadogo. Alifariki mwaka 2019 akiwa jela katika kile kilichotajwa kuwa alijiua, kitendo kilichozidisha nadharia ya njama dhidi yake.