BUDAPEST: Maadhimisho ya mapinduzi ya mwaka 1956 nchini Hungary, yachafuliwa na maandamano ya upinzani | Habari za Ulimwengu | DW | 24.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BUDAPEST: Maadhimisho ya mapinduzi ya mwaka 1956 nchini Hungary, yachafuliwa na maandamano ya upinzani

Maandamano dhidi ya serikali ya Hungary yameathiri maadhimisho ya mwaka wa 50 tangu kuanguka kwa utawala wa kikoministi mwaka wa 1956. Polisi wamelazimika kutumia gesi za kutoa machozi na risase za mpira kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Budapest. Kwa uchache watu 128 wamejeruhiwa na wengine kiasi ya 100 wamekamatwa na kuzuwilia na polisi.

Purkushani imeendelea hadi leo asubuhi. Wajumbe kutoka nchi 50 wamehudhuria sherehe za maadhimisho hayo ya mapinduzi ya mwaka 1956. Sherehe zimefanyika mbele ya jengo la bunge. Ujerumani imewakilishwa na rais Horst Köhler.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com