Berlin. Uvataji sigara utaamuliwa na majimbo. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin. Uvataji sigara utaamuliwa na majimbo.

Serikali ya Ujerumani imethibitisha ripoti kuwa itapunguza makali mipango ya kupiga marufuku nchi nzima uvutaji wa sigara. Pendekezo lililotolewa na kundi linaloangalia jinsi ya kuzuwia uvutaji wa sigara katika majengo yote ya umma, hospitali na mikahawa litapunguzwa makali baada ya serikali kueleza wasi wasi wake kuwa marufuku hiyo inaweza kwenda kinyume na katiba.

Itakuwa sasa jukumu la majimbo 16 ya Ujerumani kutekeleza marufuku hiyo kama watakavyoona kuwa sawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com