Belfast:Kikao cha majadiliano juu ya kugawana madaraka chavunjika.
24 Novemba 2006Matangazo
Kikao cha kwanza cha kujadili mipango ya kugawana madaraka kati ya vyama vya kisiasa huko Ireland kaskazini kiliahirishwa leo, pale muuaji mmoja maarufu wa kundi la zamani la wanamgambo wa kiprotestanti aliporusha zana fulani ya moshi, ndani ya jengo la bunge.
Michael Stone aliwahiwa na walinzi wa usalama mlangoni na hakuna aliyejeruhiwa.
Tukio hilo limekuja katika wakati ambapo vyama vya kisiasa mkoani humo, vikikutana kujaribu kufikia makubaliano juu ya kugawana madaraka kati ya waprotestanti wanaopendelea kuendelea kwa utawala wa kiingereza na chama cha Sinn Fein (Shin Fen) kinachopigania Ireland iliyo moja, yaani muungano na Jamhuri ya Ireland.