BAGHDAD: Moqtada al Sadr bado yumo Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 14.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Moqtada al Sadr bado yumo Irak

Wapambe wa shehe wa kishia Moqatada la Sadr wamesema shehe huyo yumo Irak.

Hapo awali iliripotiwa kwamba Moqtada al Sadr, amekimbia Irak kwenda Iran. Kuondoka kwa al Sadr kumehusishwa na mpango wa rais Bush wa kuongeza wanajeshi 21,500 nchini Irak. Marekani imelitaja jeshi la Mehdi la Moqtada al Sadr, kama tisho kubwa kwa usalama wa Irak na imemtaka waziri mkuu wa Irak, Nuri al Maliki, alipokonye silaha.

Ripoti ya kukimbia kwa al Sadr imetolewa siku chache baada ya maofisa wa jeshi la Marekani mjini Baghdad kuwaonyesha waandishi wa habari makasha ya silaha walizosema zimetengenezwa nchini Iran na kusema maofisa ngazi ya juu katika serikali ya Iran wanahusika katika kuwapa silaha wapiganaji wa Irak.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com