1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock aendeleza ziara yake katika mataifa ya Scandinavia

Amina Mjahid
14 Februari 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock anatarajiwa kuwasili nchini Sweden leo Jumanne ikiwa ni siku ya mwisho za ziara yake ya siku mbili katika mataifa ya Scandinavia.

https://p.dw.com/p/4NSEs
Finnland Besuch Außenministerin Baerbock in Helsinki
Picha: Christophe Gateau/dpa/picture alliance

Mazungumzo yake na mwenzake wa Sweden, Tobias Bill-ström, mjini Stockholm yatatuwama katika mpango wa taifa hilo kujiunga na Jumuiya ya Kujihami NATO. 

Sweden inataka kujiunga na muungano huo wa kijeshi wa mataifaya Magharibi pamoja na Finland ambayo Baerbock aliitembelea hapo jana.

Soma pia:Baerbock aanza ziara ya siku mbili Finland, Sweden

Vita vya Urusi nchini Ukraine vilisababisha mataifa hayo mawili wanachama wa Umoja wa Ulaya kutaka kujiunga na NATO mwaka  2022. 

Mataifa yote 30 yanayounda muungano huo wa kijeshi yanapaswa kuidhinisha hilo. Hungary na Uturuki zinaendelea kupinga hilo.