ANKARA: Uturuki imeahidiwa msaada kupambana na PKK | Habari za Ulimwengu | DW | 03.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA: Uturuki imeahidiwa msaada kupambana na PKK

Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice ameahidi kuisaidia Uturuki katika vita vyake dhidi ya chama cha Kikurd PKK kilichopigwa marufuku.Baada ya majadiliano yake pamoja na Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan na Waziri wa Nje Ali Babacan wa Uturuki,Bibi Rice alisema,PKK ni adui wao wote.

Maelezo zaidi ya msaada huo yatajadiliwa siku ya Jumatatu pale Waziri Mkuu Erdogan atakapokutana na Rais George W.Bush wa Marekani mjini Washington.

Wanamgambo wa PKK huitumia kaskazini ya Irak kuishambulia Uturuki.Sasa Uturuki imepeleka kiasi ya wanajeshi 100,000 kwenye mpaka wake na Irak, ikijitayarisha kwa uwezekano wa kuvishambulia vituo vya wanamgambo wa PKK kaskazini mwa Irak. Washington na Baghdad zimetoa mwito kwa Ankara kutochukua hatua ya kijeshi kwa hofu kuwa itasababisha machafuko katika eneo pekee lenye utulivu wa aina fulani nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com