Al-Shabaab yaapa kupinga Israel kuitambua Somaliland
27 Desemba 2025
Matangazo
Msemaji wa kundi hilo Ali Dheere amesema hatua ya Israel kuitambua Somaliland kama taifa huru inaonyesha kuwa Tel Aviv imeamua kupanua udhibiti wake katika maeneo ya Somalia ili kuunga mkono kile ilichokitaja kama "utawala wa watu wanaokwenda kinyume na misingi ya kidini" katika maeneo ya kaskazini-magharibi.
Somaliland haijawahi kutambuliwa rasmi na nchi yoyote, jambo lililoiweka katika hali ya kutengwa kisiasa na kiuchumi licha ya kuwa katika moja ya njia muhimu zaidi za biashara duniani zinazounganisha Bahari ya Hindi na Mfereji wa Suez.