1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky kufanya ziara Uturuki na kukutana na Erdogan

Sylvia Mwehozi
8 Machi 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atazuru Uturuki leo Ijumaa kwa mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdogan kuhusu vita dhidi ya Urusi na usafirishaji katika Bahari Nyeusi.

https://p.dw.com/p/4dI5i
Volodymyr Zelensky |  Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan 2023Picha: Presidency of Turkey/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky atazuru Uturuki leo Ijumaa kwa mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdogan kuhusu vita dhidi ya Urusi na usafirishaji katika Bahari Nyeusi.

Ofisi ya rais wa Uturuki imesema vita vya Urusi na Ukraine na kuanzishwa upya kwa ukanda salama katika Bahari Nyeusi, ni miongoni ajenda za mazungumzo ya marais hao. Mara ya mwisho kwa Zelensky kuizuru Uturuki ilikuwa ni Julai 2023 alipofanya mazungumzo ya kina na Erdogan.

Uturuki, ambayo inaitegemea sana Urusi katika usambazaji wa nishati, imekwepa kujiunga na vikwazo dhidi ya Moscow na mara kwa mara inashutumiwa na Mataifa ya magharibi kwa kuvikwepa.

Lakini taifa hilo kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, lilifanikisha makubaliano kati ya Urusi na Ukraine ambayo yaliruhusu usafirishaji wa nafaka za Kyiv kupitia Bahari Nyeusi hadi Urusi ilipojiondoa mnamo Julai 2022.