Will al Bashir be tried at all? | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.07.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Will al Bashir be tried at all?

Jee rais wa Sudan al Bashir atafunguliwa mashtaka?

Maafa yanayotokea katika jimbo la Darfur

Maafa yanayotokea katika jimbo la Darfur

Hatua ya kumfungulia mashtaka rais Omar Al Bashir wa Sudan ambae bado yupo madarakani inatishia kuigawanya jumuiya ya kimataifa. Nchi za magharibi zinataka rais huyo ajibu mashtaka juu ya mauaji halaiki wakati Urusi na China zinapinga.

Iwapo rais Omar al bashiri atafikishwa mahakamni kujibu mashtaka hayo, hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi aliepo madarakani kufanyiwa hivyo.

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa inayopamabna na uhalifu Luis Moreno Ocampo- ICC ya mjini tha Hague amewasilisha ushahidi kutthibisha kuwa rais al Bashiri ametenda uhalifu wa mauaji halaiki katika jimbo la Darfur.Ushahidi huo ulifutia miaka mitatu baada ya Baraza la usalamaa la Umoja wa Mataifa kumpa jukumu la kuchungunza mashtaka. Kinachosubiriwa sasa ni kutolewa hati ya kisheria ili rais al bashiri aweze kukamatwa.

Hatahivyo mwendesha mashtaka amewasilisha ombi kwa mahakimu 18 wanaokwakiliosha kanda tarkiban zote za dunia.

Wanaweza kukubali aua kukataa kama anavyosema mwndesha mastka mwenyewe Luis Moreno Ocampo.

OTON.

Nimetoa ombi kutaka umamuzi wa mahakimu.Wanaweza kukubali ombi langu ama wanaweza kulikataa, au wanaweza kudai ushahidi zaidi.Mahakimu sasa ndio wenye mamlaka ya kuamua."

Lakini utaratibu huo unaweza kuchukua miezi kadhaa kutokana na sababu za kisiasa hasa kwa kuzinagtia kwamba al bashiri ni mkuu wa nchi ya kiafrika. kama navyosisitiza yeyev mwenyewe.

OTON Bashir.

Chini ya ibara ya 16 ya mkataba wa Rome uliowezesha kuundwa mahakama ya kimataifa ya ICC, baraza la Usalama la Umoja wa Mataiafa lina mamlaka ya kuzuia mashtaka yoyote dhidi ya rais al bashiri kwa kipindi cha miezi 12. Baraza la Usalama linaweza kutoa ombi hilo kwa maranyingine kwa kutumia hoja zilezile. Hakuna uchunguzi au mashtaak yanayoweza kufunguliwa ikiwa ibara hiyo ya 16 itatumiwa na baraza la usalama.

Mwakilshi mmoja wa kibalozi amesema, kuwa China na Urusi, zilizopinga vikwazo dhidi ya Zimbabwe wiki jana huenda zikaamua kutopiga kura ikiwa Marekani,Ufaransa na Uingereza zitatoa hakikisho kwamba baraza ya usalama halitaunga mkono mashtaka dhidi ya rais Al -Bashir....

Ikiwa mahakama ya kimataifa ya ICC itatoa hati ya kuwezezsha kukamatwa kwa rais Omar alBashir , hatua hiyo itakuwa na athari za kisiasaa na kkijeshi na huivyo kuvuruga juhudi za amani zinazoendlea sasa nchini Sudan. Hatua ya mahakama ya kimataifa pia inaweza kuhatarisha usalama wa wanajeshsi alfu 9 wa Umoja wa mataifa na Umoja wa afrika wanaolinda amani nchini Sudan.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kimoon ambae amepitsha juhudi kubwa za kuleta amani nchini Sudan amejiweka kandoa na maamuzi ya mahakama ya kimataifa na ya mwendesha mashtaka wake mkuu.

Katibu mkuu amesema mahakama ya kuu y a ICC ni taasisi huru na kwamba Umoja wa mataifa unapaaswa kuheshimnu maamuzi ya kisheria.

Baadhi ya watalamu wa sheria wansema hataua ya mahakama ya kimataifa imekuja wakati mbaya. Mtaalamu mmoja amesemakuwa hakuna shaka kwamba rais al bashir ana husika na matukio ya Darfur, hatahiyvo mashtaka ya mahakama kuu y a kimataifa hayatasaidia katika juhudi za kuleta amani nchini Sudan.

Msimamo huo umesisiitizwa pia na Umoja wa Afrika.Umoja huo umesema haki itendeke bila ya kuzuia juhudi za amani.


 • Tarehe 15.07.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Ed3C
 • Tarehe 15.07.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Ed3C
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com