1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Watu wawili wauawa katika shambulizi la bunduki Marekani

Bruce Amani
3 Julai 2023

Maafisa wa Baltimore, jimbo la Maryland, nchini Marekani, wanaendelea kuwatafuta washukiwa wa shambulizi la ufyatuaji risasi lililotokea mapema Jumapili.

https://p.dw.com/p/4TLHx
USA | Massenschießerei in Baltimore
Picha: Kyle Mazza/NurPhoto/IMAGO

Watu wawili waliuawa na wengine 28 kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi wakati wa sherehe kwenye mtaa mwa mji huo, wa Brooklyn Homes. Meya wa Baltimore Brandon Scott amesema tukio hilo linaangazia umuhimu wa kushughulikia tatizo la umiliki wa bunduki, siyo mjini humo pekee mbali kote nchini.

Soma zaidi: Watu kadhaa wauwawa kwa kupigwa risasi Texas, Marekani

Katika hotuba yake, Meya Scott alisema hawatapumzika hadi waliofanya ukatili huo watakapotiwa mbaroni.

Maafisa wamesema karibu watu wawili walifyatua risasi kwenye shambulizi hilo, lakini huenda idadi ya waliohusika ikawa kubwa Zaidi.