1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadhaa wauwawa kwa risasi Texas, Marekani

7 Mei 2023

Watu tisa wameuliwa baada ya kupigwa risasi na mtu aliyekuwa na bunduki katika mji wa Allen kwenye jimbo la Texas nchini Marekani. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa katika shambulio hilo.

https://p.dw.com/p/4R0Me

Watu tisa wameuliwa baada ya kupigwa risasi na mtu aliyekuwa na bunduki katika mji wa Allen kwenye jimbo la Texas nchini Marekani. Watu wengine kadhaa walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Watatu miongoni mwao wamo katika hali mbaya. Kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari, miongoni mwa waliouawa ni watoto waliokuwa na umri wa miaka mitano. Anayetuhumiwa kuwa mshambuliaji naye aliuliwa kwa kupigwa risasi na polisi. Mtu huyo alifyatua risasi kwenye sehemu ya maduka. Mauaji kama hayo yanatokea mara kwa mara nchini Marekani ambako idadi ya bunduki inapita ile ya watu. Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya takwimu za mashambulio ya bunduki nchini Marekani, mauaji kama hayo yameshatokea zaidi ya mara 195 mnamo mwaka huu hadi sasa.