Watu 5 wapigwa risasi na kuuwawa na polisi Watamu Kenya
31 Machi 2010Matangazo
Nchini Kenya watu watano wameuawa na wengine wasiopungua 17 kulazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya risasi, kufuatia vurugu iliotokea baina ya wanakijiji wa Watamu mjini Malindi na maafisa wa usalama.
Wingu la simanzi lilitanda katika kijiji hicho maarufu sana kwa shughuli za kitalii wakati wa maziko ya baadhi ya waliouawa.