1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 36 wamekufa baada ya jengo la kanisa kuanguka Ethiopia

1 Oktoba 2025

Watu wapatao 36 wamekufa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa baada ya kanisa lililokuwa likiendelea kujengwa kuanguka Jumatano kwenye mji wa Arerti, Ethiopia.

https://p.dw.com/p/51MFi
Äthiopien Mekelle | Katholische Kirche St. Marien
Picha: Million Hailesilassie/DW

Mkuu wa Polisi wa Arerti, Ahmed Gebeyehu amesema idadi ya vifo inaweza ikaongezeka, kwani baadhi ya watu bado wamekwama kwenye vifusi.

Watu waliojeruhiwa vibaya wamepelekwa hospitali kwenye mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Ajali hiyo imetokea wakati ambapo kundi la waumini walikuwa wanahudhuria sherehe za kila mwaka za Bikira Maria.

Seyoum Altaye, daktari katika hospitali moja ya eneo hilo, amesema waathirika ni pamoja na watoto na wazee.

Amesema hospitali hiyo inatafuta msaada kutoka kwa Shirika la Msalaba Mwekundu, ili kuwashughulikia watu waliojeruhiwa