1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja afa katika shambulio la bunduki Marekani

Sylvia Mwehozi
15 Februari 2024

Watoto wanane ni miongoni mwa watu 22 waliojeruhiwa katika shambulio la ufyatuaji risasi mjini Kansas nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/4cPex
Kansas City
Watu wa huduma ya dharura wakiwasili eneo la mkasa wa shambulio la bundukiPicha: Charlie Riedel/AP/picture alliance

Watoto wanane ni miongoni mwa watu 22 waliojeruhiwa katika shambulio la ufyatuaji risasi mjini Kansas nchini Marekani.  Shambulio hilo limetokea wakati wa gwaride la kusherehekea ushindi wa timu ya Kansas ya Chiefs katika tamasha la Super Bowl.

Soma habari kama hii: Watu wawili wauawa, wengine kadhaa wajeruhiwa katika shambulizi la bunduki Baltimore

Mtu mmoja anaripotiwa kupoteza maisha katika mkasa huo ambao umeshuhudia mashabiki waliojawa na hofu wakikimbia kujificha, wakati wa ufyatuaji risasi. Mkuu wa polisi wa eneo hilo Stacey Graves, amesema kuwa wanawashikilia watu watatu na tayari uchunguzi umeanza.

Shambulizi hilo limetokea karibu na karakana ya kuegesha magari ambapo umati mkubwa wa watu ulikuwa umekusanyika wakati wachezaji na wafanyakazi wa timu wakipanda jukwaani kusherehekea ushindi.