1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON :Kiwanda cha Yongbyong kutathminiwa

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiB

Marekani inaandaa tathmini kamili ya mpango wa nuklia ya Korea Kaskazini baada ya kutangaza kuwa imefunga kiwanda chake pekee cha nuklia cha Yongbyon.Kulingana na mshauri wa kitaifa wa usalama wa Marekani Stephen Hardley kundi la waangalizi wa Umoja wa Mataifa wanajiandaa kuthibitisha tangazo hilo.

Kundi la waangalizi 10 waliwasili nchini Korea Kaskazini siku ya Jumamosi kuhakikisha kuwa kiwanda hicho cha nuklia kilicho umbali wa kilomita 100 kutoka mji mkuu kimefungwa.Hii ni hatua ya kwanza ya Korea Kaskazini kumaliza mpango wake wa nuklia.

Wakati huohuo Korea Kusini inapeleka mafuta nchini humo hii leo katika mpango wa kusitisha mpango wake wa nuklia.

Mwezi Februari Korea Kaskazini,Kusini,Marekani,Japan,Urusi na Uchina zilifikia makubaliano ya kuisaidia Korea Kaskazini kwa mafuta baada ya kusitisha mpango wake wa nuklia.

Mazungumzo ya pande sita yanatarajiwa kuanza tena siku ya Jumatano mjini Beijing ili kujadilia awamu inayofuatia ili kusitisha mpango wa nuklia wa Korea kaskazini.