Wapinzani Tanzania wakatazwa kuandamana | Matukio ya Afrika | DW | 08.06.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wapinzani Tanzania wakatazwa kuandamana

Polisi Tanzania imepiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara ya upinzani kwa muda usiojulikana. Upinzani uliitisha mikutano ya hadhara kwa kushinikiza kile kilichoitwa kubinywa kwa demokrasia.

Sikiliza sauti 03:02

Mahojiano na Advera Bulimba wa jeshi la polisi

Hatua hii inakuja baada ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuutawanya umati wa wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA na viongozi wao mjini Kahama, Shinyanga. Upinzani uliitisha mikutano ya hadhara nchi nzima kwa kushinikiza kile unachokieleza kubinywa kwa demokrasia kunakofanywa na utawala wa Rais John Pombe Magufuli wa taifa hilo. Kufuatia hatua hiyo DW imezungumza na msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba ambaye kwanza anaelezea sababu za kuchukuliwa kwa uamuzi huo.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada