1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wang Yi aahirisha ziara yake nchini Somalia

Josephat Charo
9 Januari 2026

Wizara ya mambo ya nje ya Somalia imetangaza Ijumaa kwamba mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi ameahirisha ziara yake iliyokuwa imepangwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/56bJU
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ameahirisha ziara yake nchini Somalia.
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ameahirisha ziara yake nchini Somalia.Picha: dts-Agentur/picture alliance

Maafisa wa ngazi ya juu katika wizara hiyo wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba sababu ya kuahirishwa kwa ziara ya Wang Yi nchini Somalia na tarehe nyingine itakapofanyika, itatolewa baadaye.

Wang Yi alikutana na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Alhamisi na kutoa wito pawepo ushirikiano mkubwa zaidi na nchi hiyo ya Afrika ambayo uchumi wake unakua kwa kasi kabisa, ikiwemo miundombinu, nishati safi isiyochafua mazingira na uchumi wa kidijitali.

Wang Yi alikutana na Abiy mjini Addis Ababa katika kituo chake cha kwanza cha ziara yake ya kila mwaka ya mwaka mpya ya siku sita hadi Januari 12 barani Afrika, itakayompeleka pia Tanzania na Lesotho.