1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Wahouthi waidungua droni ya Marekani

21 Mei 2024

Wahouthi wa Yemen wameidungua droni ya Marekani chapa MQ9 katika anga la mkoa wa al Bayda kusini mwa Yemen.

https://p.dw.com/p/4g6C1
Jemen I Parade von Houthi-Anhängern im Jemen aus Protest gegen Angriffe der USA und Großbritanniens
Picha: Mohammed Hamoud/Anadolu/picture alliance

Hayo yamesemwa na Yahya Saree, msemaji wa kundi hilo la waasi linaloegemea Iran katika hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Saree amesema droni hiyo ililengwa na kombora la kutokea ardhini kwenda angani na kwamba video kuthibitisha madai hayo zitatolewa.

Wahouthi walisema siku ya Ijumaa waliidungua droni nyingine ya Marekani aina kama hiyo katika anga la mkoa wa kusini mashariki wa Maareb.

Kundi wa Wahouthi linaloudhibiti mji mkuu Sanaa na maeneo mengi ya Yemen limezishambulia meli katika bahari ya Shamu tangu mwezi Novemba mwaka uliopita kuonyesha mshikamano na Wapalestina katika vita kati ya Israel na kundi la Hamas.