Wafungwa 25 wapigwa risasi na kuuwawa na polisi nchini Syria | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wafungwa 25 wapigwa risasi na kuuwawa na polisi nchini Syria

-

Takriban wafungwa 25 wamepigwa risasi na kuuwawa hii leo na vikosi vya usalama vya Syria wakati wa maandamano yaliyotokea kwenye jela ya wafungwa wa kisiasa nchini humo katika eneo la milimani nje ya mji mkuu Damascus.Taarifa hizo zimetolewa na waangalizi wa kundi moja la kutetea haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza.

Kundi hilo la kutetea haki za binadmu limefahamisha kwamba mauaji yanaendelea katika jela hiyo na wafungwa kadhaa wamepanda juu ya gereza la kijeshi katika eneo la Saydnaya kaskazini mwa Damscus kutoroka ghasia hizo.Aidha kundi hilo limesema jamaa za wafungwa kadhaa wamepiga simu kumuomba rais Bashar al Assad kuingilia kati ghasia hizo na kuzuia mapigano yanayoendelea.hata hivyo hadi sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa kutoka upande wa maafisa wa serikali ya Syria.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com