Wacongo 8000 wakimbilia Uganda ndani ya mwezi mmoja | Matukio ya Afrika | DW | 03.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wacongo 8000 wakimbilia Uganda ndani ya mwezi mmoja

Maelfu ya wakimbizi wa DR Congo wanavuka ziwa Albert kwa boti na kuingia Uganda kukwepa vurugu za kikabila. Vituo vya kupokea wakimbizi vyaelemewa na msaada unapungua. Baraza la wakimbizi la Norway latoa wito wa msaada.

Ongezeko maradufu la idadi ya wakimbizi wanaoingia Uganda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, limesababisha mashaka kuhusiana na shughuli za kuwahudumia.

Mashirika ya huduma kwa wakimbizi pamoja na serikali ya Uganda wanaelezea kwamba ikiwa mwenendo huu utaendelea bila wahisani kutoa misaada, hawataweza kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao.

"Wakimbizi zaidi wanawasili Uganda kutoka DR Congo, na mwisho wa hali hii haujulikani. Hili limesababisha uhaba wa msaada wa dharura, suala linalotishia afya na maisha ya wakimbizi," alisema Kaimu Mkurugenzi Mkaazi wa Baraza la Wakimbizi la Noeway (NRC), Melchizedeck Malile.

Kulingana na takwimu za Bbraza hilo, idadi ya wakimbizi waliovuka mpaka kutoka DRC na kuingia Uganda mwezi wa Juni imeongezeka kutokana na ghasia za kikabila pamoja na ugonjwa wa Ebola.

Logo NCR

Baraza la wakimbizi la Norway limeeleza wasiwasi kuhusu idadi inayoongozeka ya wakimbizi wa DRC nchini Uganda, huku msaada kwa wakimbizi ukizidi kupungua.

 

Katika taarifa yake ya kila mwezi, Baraza la Norway la wakimbizi linakadiria kuwa zaidi ya wakimbizi 3,000 walivuka mpaka kwa mitumbwi kutoka Congo katika mwezi mmoja tu.

Vituo vya kupokea wakimbizi Uganda vyaelemewa

Vituo vya kupokelea wakimbizi nchini Uganda vinaelemewa kutokana na wimbi hili jipya. Katika mwezi uliotangulia, wasatani wa idadi ya kila siku ulikuwa wakimbizi 145 kwa siku. Tangu wakati huo, idadi ya wakimbizi wanaowasili imeonegezeka maradufu hadi kufikia 302 kwa siku.

"Kwa nogezeko hili jipya la wakimbizi wanaowasili, tunayasihi mashirika ya hisani ya kimataifa na jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada kwa wakimbizi nchini Uganda. Wakimbizi wanaowasili wanahitaji msaada wa haraka wa malaazi, maji safi na huduma za usafi. Tukiwa na ufadhili zaidi, tutaweza kuokoa maisha zaidi," anasema Malile.

Mpango wa wakimbizi wa mwaka 2019 kwa ajili ya Uganda unaomba kiasi cha dola bilioni 1.03 katika msaada wa kiutu, lakini ni dola milioni 147 tu kwa ajili ya programu za kiutu ndyio umetolewa mpaka sasa.

Karte Kongo Uganda Ituri Flüchtlinge ENG

Maelfu ya wakimbizi wamekuwa wakivuka mpaka na kuingia Uganda kwa kutumia mitumbwi kupitia Ziwa Albert, lililopo kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Nakisi za nyuma katika ufadhili zimesababisha kufungwa kwa programu za kuokoa maisha. Bila kuongeza msaada, programu zaidi zitakosa msaada unaohitajika sana kama vile chakula, malazi na maji safi na huduma za kiafaya.

Msaada wa dharura kwa Uganda

Wakati ambapo barala la Ulaya na Marekani zinaendelea kuwakataa wakimbizi na waomba hifadhi, Uganda inaendelea kuwakubali. Taifa hilo dogo lisilo na njia ya bahari linahifadhi karibu wakimbizi milioni 1.3 kwa sasa, wengi wao kutoka Sudan Kusini, DRC na Burundi.

"Uganda ina baadhi ya sheria nzuri na sera kuhusu wakimbizi duniani lakini maombi yake ya msaada zaidi hayazingatiwi, na maombi ya msaada yanaendelea kupita bila kupata ufadhili wa kutosha. Mataifa tajiri zaidi yanahitaji kutimiza ahadi zao na wajibu wa kugawana mzigo.

Mataifa kama Uganda  yanapambana kumudu hali kadiri yawezavyo, na yanahitaji rasilimali za dharura kuyawezesha kupunguza mateso ya wakimbizi," aliongeza  Malile.