1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Nordic wataka kuisadia zaidi Ukraine kivita

14 Mei 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz leo Jumanne atakutana na waziri mkuu wa Sweden Ulf Kristersson katika mazungumzo ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4fq9w
Kansela Scholz nchini Sweden
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Swedena Ulf KristerssonPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Scholz ambaye yuko ziarani Sweden jana alikuwa na mazungumzo na viongozi wa mataifa ya Ukanda wa Nordic ambapo aliyatolea mwito mataifa ya Ulaya kuiongezea msaada wa kijeshi Ukraine na hasa mifumo ya ulinzi wa anga, katika wakati nchi hiyo ikipambana kuyakabili mashambulizi ya Urusi katika eneo lake la Kaskazini Mashariki. Kansela Scholz amezisifu pia Finnland na Sweden kwa kujiunga na jumuiya ya NATO,  Zaidi alisema "Kuna tofauti moja kubwa kati ya sasa na mara ya mwisho nilipohudhuria kikao kama hichi. Hivi sasa sote ni washirika ndani ya jumuiya ya NATO kama ilivyokwishatajwa. Hii imesababishwa moja kwa moja na uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine na kurudi kwa ubeberu wa Urusi barani Ulaya.Uanachama wa Finnland na Sweden katika muungano wa NATO unauimarisha muungano huo na ni mafanikio kwa usalama wetu sote". KanselaOlaf Scholz na mawaziri wakuu wa mataifa ya  Ukanda wa Nordic, Sweden,Denmark,Finland,Iceland na Norway katika mazungumzo yao mjini Stolkholm, walikubaliana kuongeza msaada wa silaha kuisaidia Ukraine.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW