1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Vikosi vya Ukraine vyajiondoa katika mji wa Avdiivka

Sylvia Mwehozi
17 Februari 2024

Vikosi vya Ukraine vimejiondoa katika mji wa mashariki wa Avdiivka, ambako hali imezidi kuwa mbaya zaidi katika siku za hivi karibuni, amesema kamanda anayeongoza vikosi katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4cVkJ
Ukraine Militärische Mobilität ukrainischer Soldaten in Richtung Avdiivka
Picha: Ozge Elif Kizil/Anadolu/picture alliance

Vikosi vya Ukraine vimejiondoa katika mji wa mashariki wa Avdiivka, ambako hali imezidi kuwa mbaya zaidi katika siku za hivi karibuni. Taarifa hizo zimethibitishwa na kamanda wa kijeshi anayeongoza vikosi vya Ukraine katika eneo hilo Oleksandr Tarnavsky.

Afisa huyo ameandika katika mtandao wa Telegram kwamba kwa kuzingatia hali ya operesheni katika mji wa Avdiivka, ameamua kuviondoa vikosi vyake kutoka mji huo na kusogea kwenye maeneo mengine zaidi ya ulinzi ili kuepuka kuzingirwa na kuokoa maisha na afya za askari.

Kuondoka kwa wanajeshi Ukraine kutoka mjini Avdiivka, kunafuatia miezi kadhaa ya mashambulizi makali ya Urusi. Na pia kunaashiria mabadiliko makubwa zaidi katika uwanja wa mapambano tangu wanajeshi wa Urusi walipouteka mji wa Bakhmut mnamo Mei mwaka jana.