Vikosi vya Syria vyaendelea kutumia mabavu
3 Septemba 2011Matangazo
Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Syria, watu 8 wameuawa, baada ya vikosi vya usalama kuingilia kati kuyavunja maandamano katika viunga kadhaa vya mji mkuu Damascus. Wengine 6 waliuawa katika mji wa Homs ulio ngome ya uasi na 3 katika mji wa Deir Ezzor, mashariki mwa nchi hiyo.
Wakati huo huo, serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubaliana kupiga marufuku kuagiza mafuta kutoka Syria. Lengo ni kumshinikiza Assad kuacha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani wa serikali. Hatua hiyo ya marufuku imepangwa kuanza Novemba 15. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa , zaidi ya watu 2,000 wameuawa tangu maandamano ya upinzani kuanza katikati ya mwezi wa Machi katika sehemu mbali mbali nchini Syria.