1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yaapa kuendeleza mashambulizi dhidi ya Ukraine

25 Septemba 2025

Urusi imeapa kuendeleza mashambulizi yake ya kijeshi nchini Ukraine na kupuuzilia mbali madai ya Rais Donald Trump kwamba jeshi la Kiev linaweza kuyarejesha tena maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya Moscow.

https://p.dw.com/p/5125j
USA New York 2025 | Volodymyr Zelenskyy katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa MataifaPicha: Bianca Otero/ZUMA/picture alliance

Urusi imeapa kuendeleza mashambulizi yake ya kijeshi nchini Ukraine na kupuuzilia mbali madai ya Rais Donald Trump kwamba jeshi la Kiev linaweza kuyarejesha tena maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya Moscow. Rais Trump aliitaja Urusi kuwa chui asiye na meno na kusema anaamini Ukraine inaweza kurejesha kila kipande cha ardhi kilichotekwa na vikosi vya Mosow.

Matamshi ya Trump yalifuatia mazungumzo yake na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kando mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa, yalikuwa ni mabadiliko makubwa katika msimamo wake kuhusu mzozo huo wa miaka mitatu na nusu sasa, ambao wakati anaingia madarakani alijigamba kwamba angeumaliza ndani ya saa kadhaa. Jeshi la Urusi linashikilia karibu asilimia 20 ya ardhi ya Ukraine, ikijumuisha rasi ya Crimea iliyonyakuliwa mwaka 2014.