1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

UN yaitaka Uingereza kutowapeleka wahamiaji Rwanda

29 Machi 2024

Kamati ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa imeitolewa wito Uingereza kuachana na muswada wake wenye utata wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda

https://p.dw.com/p/4eF3I
Mpango wa Uingereza kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda
Mpango wa Uingereza kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda umekuwa ukipingwa vikali na Mahakama mjini LondonPicha: Niklas Halle'n/AFP/ Getty Images

Kamati hiyo imesema inaitaka serikali mjini London kusitisha mswada huo au kuufuta kabisa iwapo utapitishwa na kwamba imesikitishwa na makubaliano ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa muswada huo unaoweza kuwa sheria mwezi ujao, na kusema makubaliano kati ya nchi hizo hayakujali uamuzi wa Mahakama Kuu ya Uingereza iliyosema kuwa mpango huo unakinzana na sheria za kimataifa.

Soma pia: Uingereza ingali na lengo kuwapeleka wakimbizi Rwanda

Serikali ya kihafidhina ya Waziri Mkuu Rishi Sunak inalenga kuanzisha mpango huo ili kuwakatisha tamaa maelfu ya wahamiaji wanaowasili Uingereza kwa kutumia mashua ndogo, lakini vikwazo vya kisheria vimekuwa vikiuzuia muswada huo.