1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

UN: 26% ya watu duniani hawana maji safi

22 Machi 2023

Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji unaanza Jumatano huko New York, Marekani, huku ripoti iliyozinduliwa Jumanne ikisema asilimia 26 ya watu duniani hawapati maji safi ya kunywa.

https://p.dw.com/p/4P3JQ
Themenpaket | Weltwasserbericht Themenbild Wassermangel Dürre Trinkwasser
Picha: Thomas Schulze/picture alliance

Inaripotiwa kwamba asilimia 46 ya watu duniani aidha hawawezi kufanya usafi wa msingi kutokana na ukosefu au uhaba wa maji.

Ripoti hiyo inatahadharisha kwamba dunia hivi karibuni itakabiliwa na mzozo wa maji.

Mkutano huo mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji unafanyika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45 na mhariri mkuu wa ripoti hiyo iliyozinduliwa Richard Connor, anasema matumizi ya maji kote duniani yameongezeka kwa karibu asilimia moja kwa mwaka katika kipindi cha miongo minne iliyopita.

Watu bilioni 3.5 wakabiliwa na uhaba wa maji

Connor anasema ili kukabiliana na hali hiyo, binadamuwamekuwa wakitafuta maji ya chini ya ardhi kwa kuchimba visima zaidi, hatua iliyopelekea kupotea kwa kati ya mapipa trilioni 26 hadi 52 ya hifadhi za maji kila mwaka.

Themenpaket | Weltwasserbericht Themenbild Wassermangel Dürre Trinkwasser
Msichana huko India akisubiri kuteka majiPicha: Tsering Topgyal/dpa/picture alliance

"Asilimia kumi ya idadi jumla ya watu duniani kwa sasa wanaishi katika sehemu ambazo zina matatizo makubwa ya maji. Katika ripoti yetu, tulisema hadi watu bilioni 3.5 wanaishi katika hali ya uhaba au matatizo ya maji kwa takriban mwezi mmoja kila mwaka," alisema Connor.

Ripoti hiyo imetoa picha ya pengo kubwa linalohitajika kujazwa ili kuyafikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha watu wote wanapata maji safi na ifikiapo mwaka 2030. Connor amesema makadirio ya thamani ya kuyafikia malengo hayo ni kati ya bilioni 600 hadi trilioni moja kila mwaka.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kwamba uhitaji unaoongezeka wa maji unashuhudiwa katika nchi zinazoendelea na zenye uchumi unaokuwa kutokana na ongezeko la viwanda na idadi ya watu inayoongezeka mijini.

Watu walio na matatizo ya maji mijini watarajiwa kuongezeka

ya matumizi ya maji duniani ila kadri idadi ya watu katika miji inavyozidi kuongezeka, mkakati unaotumika sana sasa hivi ni kuyaondoa maji kutoka kwenye kilimo na kuyapeleka katika maeneo ya mijini.

Upatikanaji wa Maji Safi na Salama

Ila mkakati huo hautarijiwi kukidhi mahitaji kwa kuwa idadi ya wakaazi wa mijini wanaokabiliwa na kitisho cha maji inatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 933 kama ilivyokuwa mwaka 2016 hadi kati ya bilioni 1.7 na bilioni 2.4 mwaka 2050.

Umoja wa Mataifa vile vile umesema mabadiliko ya tabia nchi yatapelekea uhaba wa maji wa misimu kuongezeka katika maeneo ambayo yana maji kwa wingi kwa sasa kama Afrika ya Kati, Asia Mashariki na sehemu za Amerika ya Kusini. Tatizo hilo litaongezeka katika maeneo ambayo tayari yanashuhudia uhaba wa maji kama Mashariki ya Kati na eneo la Sahara barani Afrika.

Vyanzo: AP/AFP