1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya yaiwekea vikwazo vya kiuchumi Belarus

24 Juni 2021

Umoja wa Ulaya siku ya Alhamisi umeiwekea vikwazo vya kiuchumi Belarus kwa kile walichokiita "ongezeko la ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu" ikiwemo kumuweka kizuizini mwandishi wa habari Raman Pratasevich.

https://p.dw.com/p/3vW6n
Belgium EU Visegrad
Picha: Francois Lenoir/AP/picture alliance

Vikwazo hivyo sio tu vinalenga uchumi wa taifa hilo, lakini pia kumkabili raisi Alexander Lukashenko na washirika wake.

Pratasevich, mwandishi wa habari mkosoaji alikamatwa Mei 23 baada ya msimamizi wa safari za ndege wa Belarus kuamrisha ndege ya Ryanair iliyokuwa safarini kutoka Ugiriki kuelekea Lithuania kutua Minsk. soma zaidi Ulaya kuiwekea Belarus vikwazo vikali zaidi

Vikwazo vilivyokubaliwa Alhamisi vinalenga viwanda, ikiwa ni pamoja na kiwanda cha mbolea, mauzo ya nje ya tumbaku na bidhaa za mafuta.

"Biashara ya bidhaa za petroli, Potasium Chloride (` potashi '), na bidhaa zinazotumiwa katika uzalishaji au utengenezaji wa bidhaa za tumbaku zimezuiliwa, " ilisema taarifa ya Umoja wa Ulaya. soma zaidi UN kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu Belarus

Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa vikwazo hivyo vinahusisha marufuku ya kuiuzia Belarus vifaa na programu zinazoweza kutumika kufuatilia mtandao wa intaneti na mawasiliano ya simu.

Vikwazo hivyo pia vinaizuwia Belarus kuyafikia masoko ya mitaji ya Umoja wa Ulaya, na vimesitisha malipo kwa sekta ya umma ya taifa hilo kutoka Benki ya uwekezaji ya Ulaya.

Data visualization: The history of Belarus' tumbling democracy - English - ONLY USE WITH DATA STORY

Umoja wa Ulaya umeongeza vikwazo dhidi ya Belarus tangu Lukashenko, anaetajwa kama dikteta aliesalia Ulaya aliposhinda urais kwa mara ya sita mnamo Agosti katika uchaguzi ambao umoja huo unautaja kuwa wa ulaghai.

Kanda hiyo yenye nchi wanachama 27, imechukua msimamo mkali zaidi tangu tukio la Ryanair, na kuhusiana na madai ya utumiaji wa mahamiaji kuitia kishindo nchi jirani ya Lithuania, ambayo imewapa hifadhi wanasiasa wa upinzani wa Belarus, na ni mmoja wa wakosoaji wakubwa zaidi wa Lukashenko.

Belarus Minsk | Präsident Alexander Lukaschenko
Alexander Lukaschenko Picha: Sergei Shelega/BelTA/AP/picture alliance

Siku ya Jumatatu, mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya waliweka marufuku ya kusafiri na kuzuwia mali za maafisa 78 wa Belarusi na 8 makampuni ambayo kawaida ni benki, au vyama.

Jumla ya watu 166 na makampuni 15 nchini Belarusi sasa ziko chini ya hatua za vikwazo vya Umoja wa Ulaya. Marekani, Uingereza na Canada pia zimewawekea vikwazo viongozi wakuu wa Belarusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema watalenga upande wa kiuchumi ambao unaathari kubwa Belarus pamoja na kipato cha utawala wake. Soma Upinzani waitisha mgomo wa taifa nchini Belarus

Hatua hii imeibua hasira kutoka Belarus, na wazara wa mambo ya nje kutoa tamko kuwa uamuzi huo utaumiza mwananchi wa kawaida na kuanzisha vita vya kiuchumi. Wizara hiyo aidha imeonya kuwa taifa hilo litalazimika kuchukua hatua za kulipiza kisasi zitakazoumiza makampuni ya magharibi.

Belarus imekumbwa na mtikisiko kwa miezi akdhaa kutokana na maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena kwa rais Lukashenko. Mamlaka ilijibu maandamano hayo kwa ukandamizaji mkubwa ambao ulisababisha zaidi ya watu 35000 kukamatwa na maelfu wengine kupigwa na polisi. Viongozi wengi wa upinzani wametiwa mbaroni au kulazimishwa kuondoka nchini humo.

Tangu alipokamtwa mwandishi wa habari Pratasevich amekuwa akionyeshwa katika vyombo vya habari vya serikali kwa machozi akiomba radhi kwa makosa yake na kumpongeza Lukashenko. Upinzani Belarus wasema mwandishi aliyekamatwa aliteswa jela

Wazazi wake, viongozi wa upinzani na watu wengine kutoka Magharibi wanaamini kuwa Pratasevich amesezungumza hayo chini ya shinikizo, na wengine wakisema kuwa alikuwa na dalili za kupigwa.

/Ap