1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu Belarus

19 Mei 2021

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusiana na haki za binadamu Michelle Bachelet amewataja wataalam 3 watakaomsaidia kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu Belarus kufuatia uchaguzi uliokuwa na utata

https://p.dw.com/p/3td7D
Michelle Bachelet | UN Hochkommissarin für Menschenrechte
Picha: picture-alliance/Keystone/S. Di Nolfi

Bachelet amemteua Karinna Moskalenko ambaye ni wakili wa haki za binadamu kutoka Urusi na ambaye atahudumu kama mwenyekiti. Mwengine aliyeteuliwa ni Susan Bazili ambaye ni wakili wa haki za binadamu kutoka Canada na Marko Milanovic ambaye ni profesa wa sheria kutoka Serbia.

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ambaye ameiongoza nchi hiyo kutoka mwaka 1994 alishinda muhula wa sita katika uchaguzi huo uliofanyika mwezi Agosti mwaka jana na ambao upinzani na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wanasema ulikumbwa na udanganyifu.

Alikabiliwa na maandamano ambapo maelfu ya waandamanaji walikamatwa na zaidi ya mia nne kupewa vifungo vya muda mrefu jela.