1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Belarus wasema mwandishi aliyekamatwa aliteswa jela

31 Mei 2021

Kiongozi wa upinzani wa Belarus Svetlana Tsikhanovskaya amesema kuwa mwanablogu anayeshikiliwa nchini Belarus Roman Protasevich amepigwa na kuteswa akiwa jela

https://p.dw.com/p/3uDXy
Belarus  - Oppositioneller Roman Protasevich in Minsk verhaftet
Picha: Artur Widak/NurPhoto/picture alliance

Wakili aliyemtembelea Protasevich na mpenzi wake Sofia Sapega alisema yuko salama ila Tsikhanovskaya amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa hiyo ni ya kutiliwa mashaka kwa kuwa ukweli ni kwamba aliteswa na kupigwa.

Kiongozi huyo wa upinzani hajatoa ushahidi kuhusiana na madai yake ingawa familia ya mwandishi huyo pia ilisema ukanda mmoja wa video kutoka jela ulionyesha dalili za mateso aliyopitia.

soma zaidi: Lukashenko azishutumu nchi za Magharibi kuanzisha vita dhidi yake

Protasevich na mpenzi wake walikamatwa mnamo Mei 23 baada ya ndege yao kulazimishwa kutua mjini Minsk.