1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhamiajiEthiopia

Umoja wa Ulaya waweka masharti magumu ya visa kwa Ethiopia

29 Aprili 2024

Umoja wa Ulaya umesema unaweka mchakato mgumu zaidi wa kupata visa kwa raia wa Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4fJVd
Italien, Messina |Wahamiaji kutoka Afrika baada ya kupokelewa kisiwa cha Sicily, Italia.
Ethiopia ni moja wapo ya mataifa ya Afrika yanatoa idadi kubwa ya watu wanaotafuta hifadhi kwenye mataifa ya kigeni.Picha: Petros Karadjias/AP/picture alliance

Hatua hiyo inafuatia kile umoja huo imekitaja kuwa ukosefu wa "ushirikiano wa kutosha" katika kuwarudisha nyumbani waomba hifadhi waliokataliwa pamoja na wahamiaji.

Hatua hiyo inamaanisha Waethiopia hawatatumia tena aina ya nyaraka wanazotoa ili kukidhi mahitaji ya maombi ya safari barani Ulaya. Hawawezi tena kupata visa ya kuingia Ulaya mara nyingi, na wanadiplomasia sasa watalazimika kulipa ada ili kupata visa.

Muda wa mchakato wa kupata visa pia umeongezwa hadi siku 45 kutoka siku 15. Sheria hizo ni sehemu ya mbinu ya Umoja wa Ulaya ya kudhibiti uhamiaji usio wa kawaida.

Umoja wa Ulaya uliweka taratibu kali kama hizo kwa  Gambia.