Umoja wa Ulaya wasaka sera ya pamoja ya nishati | Magazetini | DW | 24.11.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Uhariri wa magazeti 24.11.2016

Umoja wa Ulaya wasaka sera ya pamoja ya nishati

Juhudi za Umoja wa Ulaya za kutafuta sera ya pamoja juu ya nishati pamoja na msimamo wa rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.ndiyo waliyoyaandika wahariri waUjerumani tarehe (24.11.2016)

Gazeti la Der Neue Tag,

Ukweli wa kusikitisha ni kwamba Umoja wa Ulaya umeshindwa katika kupata msimamo wa pamoja kulinda mipaka yake pamoja na sera kuhusu wahamiaji.Kwanini basi ifikiriwe kwamba Umoja huo utafanikiwa kupata mimamo wa pamoja kuhusu sera ya nishati?Kwanini nchi hizo ziyaachie mamlaka yake ya kufanya maamuzi kwa makao makuu mjini Brussels ambayo yameshapoteza umaarufu wake?Kimoja kinachoweza kutoa tafsiri za juhudi hizi ni kwamba  matatizo yaliyopo katika usambazaji wa mafuta kwa baadhi ya nchi yataongezeka na hilo litasababisha matatizo makubwa katika tawala za nchi hizo.Je Umoja wa Ulaya utakuwa tayari kuvumilia maumivu hayo-Historia ya Umoja huo inaonesha kwamba nyingi ya nchi za Umoja huo zina uwezo mdogo wa nishati.Kwahivyo kila nchi inayendesha kivyake sera ya nishati.Kulifanya suala hilo kuwa suala la pamoja  ni kichekesho.

Gazeti la Die Rheinpfalz 

Hakuna anayeweza kuzungumzia kuhusu rais mteule wa Marekani:Yeye ni mwanaitikadi,hakuna hata mmoja anayeyajua malengo au dhamira ya kiongozi huyo,mbali na ile fikra yake ya kutaka kuifanya tena Marekani kuwa yenye nguvu kubwa.Na kwahakika hiyo ndiyo fikra pekee anayoitegemea bilionea huyo.Lakini mahojiano aliyofanyiwa katika gazeti la Newyork Times yameonesha pia kwamba ni mtu wa kubadilika kwa kiasi kikubwa.Ameonesha katika suala la mabadiliko ya tabia nchi huenda amejifunza,kuhusu watakaoathirika na mabadiliko hayo watakuwa ni wakulima wa kizungu katika eneo la kati la magharibi ikiwemo hata waliompigia kura bwana Trump.Na juu hata kwa biashara ya kilimo mambo hayotokuwa mazuri.

Gazeti la Pforzheimer 

Ikiwa wiki chache za mwanzo baada ya uchaguzi wa Marekani zimetuonesha kwamba mshindi ni mtu asiyekuwa na uzoefu wowote wa kisiasa na mitazamo yake imekuwa ikitokana sio na kitu kingine bali imekuwa ikielekea kule kwenye ujumbe aliyokuwa akiutowa kupitia Twitter.Trump anakwenda mbio kuungaunga sera zake kwa usaidizi wa washauri wake.Na kwahivyo hakuna kilichowazi bado,nikusema  wasiwasi utaendelea kuwapo.Lakini ifahamike pia  misingi ya kuuondoa wasiwasi huo itategemea wamarekani wenyewe na dunia lakini sio yeye.