Uchumi
Umoja wa Ulaya na Australia zakubaliana mkataba wa biashara
24 Machi 2026
Matangazo
Umoja wa Ulaya na Australia zimekubaliana kuhusu biashara huru baina yao.
Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, wametangaza hayo siku ya Jumanne, takriban miaka minane tangu mazungumzo hayo ya biashara huru yalipoanza.
Mkataba huo utaondoa zaidi ya asilimia 99 ya ushuru kwenye bidhaa za Umoja wa Ulaya zinazopelekwa Australia kibiashara. Hayo ni kulingana na shirika la habari la AFP.
Australia pia itapunguza ushuru kwa uagizaji wa madini muhimu.