1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya na China zakutana Bressels

Sudi Mnette
2 Juni 2017

Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang, na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya leo hii wanajiandaa kuthibitisha ahadi zao katika makubaliano ya kihistoria ya Paris, baada ya Rais Donald Trump kutangaza kujitoa.

https://p.dw.com/p/2e22D
China Jean Claude Juncker, Li Keqiang und Donald Tusk beim EU-China-Gipfel
Jean Claude Juncker, Li Keqiang und Donald Tusk Picha: picture-alliance/dpa/Pool/J. Thys

Suala la mabadiliko ya tabia nchi linatarajiwa kugubika mijadala kati ya Keqiang, ambae anaongoza ujumbe mkubwa  wa mkutano wa mawaziri, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk, na rais wa kamisheni ya umoja huo, Jean-Claude Junker, unaofanyika mjini Brussels, Ubeligiji.

Akizungumza na viongozi wa taasisi za kibiashara, akiwa pamoja na Li, Juncker amesema ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na China umefungamanishwa na kanuni zenye msingi wa mfumo wa kimataifa. Amesema Umoja wa Ulaya na China zina amini katika utekelezaji wa ukamilifu wa makubaliano ya Paris pasipo kupotosha dhima yake na kusisitiza katika jambo hilo hakutakuwa na kusitasita au kurejeshwa nyuma.

Katika mkutano wao huo, Umoja wa Ulaya na China- wachafuzi wakubwa wa mazingira duniani wanajiandaa kutoka taarifa ya pamoja, itakayothibitisha msimamo wao katika kukabiliana na ongezeko la joto duniani, kutokana na tanganzo ya Rais Trump la Alhamis. Kwa mujibu wa rasmu ya kile kinachotarajiwa kuzungumzwa pande hizo mbili zitaelezea umauzi wao katika kusonga mbele zaidi kisera na hatua katika ufanisi wa utekelezaji na hasa kufanikisha michango ya fungu la miradi ya kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi.

Matarajio ya mkutano wa kilele

Brazilien Parlament ratifiziert Pariser Klimavertrag
Bunge la Brazil liliporidhia makubaliano ya ParisPicha: picture-alliance/dpa/F. Bizerra

Vilevile kutatolewa wito wa pande zote kuzingatia makubalinao ya Paris na kuongeza jitihada kwa kuzingatia malengo na matakwa ya makubaliano.

Katika hatua tofauti na hiyo jana Alhamis, mataifa yenye nguvu barani Ulaya Ufanransa, Ujerumani na Italia kwenye taarifa yao ya pamoja yalisema yamesikitishwa na uamuzi wa Marekani wa kujiondoa katika makubaliano ya Paris, lakini pia yalithibitisha  ahadi zake katika kuteleleza hatua za makubaliano hayo na kuyatia moyo mataifa washirika kuongeza kuongeza jitihada zao katika kukabilina na mabadiliko ya taibia nchi.

Tofauti na hayo Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya Cecilia Malmstroem ameitolewa wito chini kutekeleza kanuni za pamoja za kibishara na umoja huo. Lakini tofauti zimeendelea kusalia za kwa umbali gani China itatoa fursa kwa wawekezaji wa Ulaya na biashara katika soko lake. Kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa kilele wa leo Keqiang alisisitiza kuwa China inatekeleza kanuni zilizowekwa na Shirika la Biashara Duniani-WTO.

Umoja wa Ulaya ni mshirika mkubwa wa biashara, wakati China kwa upande wau Umoja wa Ulaya unashika namba mbili. Kiwango cha biashara ni kizuri kwa pande zote mbili chenye thamani ya dola bilioni 1.68 kila siku.

Mwandishi: Sudi Mnette/Reuters/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef