1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaiomba Umoja wa Mataifa kujadili hali Mariupol

9 Mei 2022

Ukraine imetoa wito kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kufanya mkutano maalum kuijadili hali inayoendelea nchini humo hasa kuangalia hali inavyozidi kuwa mbaya mjini Mariupol.

https://p.dw.com/p/4B39o
Ukraine | Pro Russische Soldaten in Mariupol
Picha: Alexander Ermochenko/Reuters

Ukraine imetoa wito ikiwa tayari vikosi vya Urusi vimekuwa vikiendeleza mashambulizi kulenga katika maeneo muhimu na hata makaazi ya raia, hatua inayosababisha hali ya kiutu kuwa mbaya zaidi.

Balozi wa Ukraine katika Baraza la Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa Yevheniia Filipenko, ameliandikia baraza hilo akieleza yale yanayofanywa na majeshi ya Urusi katika mji muhimu wa Ukraine, Mariupol.

Katika barua hiyo ameeleza kwamba hali ya sasa inahitaji uangalizi wa dharura ikiwemo kutazama ripoti ya uhalifu wa kivita na kiwango kikubwa cha uvunjifu wa haki za binadamu, kadhalika uharibifu mkubwa mjini Bucha na maeneo mengine ambayo yamekombolewa.

Soma zaidi:Watu sitini wahofiwa kufariki Ukraine

Leo Jumatatu wizara ya ulinzi nchini Ukraine imesema kwamba vikosi vya Urusi vikiwa na vifaru pamoja na mizinga vimeendelea kufanya mashambulizi katika kiwanda cha chuma cha Azovstal ambapo bado kuna idadi yawapiganaji wa Ukraine wamejificha.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Oleksandr Motuzyanyk alithibitisha bila kutoa maelezo zaidi na kuongeza kwamba huenda vikosi vya Urusi vikafanya  mfululizo wa mashambulizi hapo baadae.

Amnesty: Urusi imefanya uhalifu Ukraine

" Adui anaendelea kutuzuia katika kituo chetu cha kiwanda cha chuma cha Azovstal" Alisema na kuongeza, kuna uwezekano wa kufanya mashambulizi mengine ya anga.

"Kuna uwezekano wa kufanya mashambulizi ya anga kwa kutumia mabomu ya masafa marefu"

Alisema bila ya kuztoa maelezo ya kina mbele ya waandishi wa habari.

Zelensky: Haturuhusu Urusi kuchukua ushindi kwa vita hivi

Akizungumza katika kumbukumbu ya ushindi wa Umoja wa Kisovieti dhidi ya majeshi ya Ujerumani iliyoongozwa na Wanazi,  Rais Volodymyr Zelensky alisema, taifa lake halitaruhusu Urusi kuchukua ushindi katika vita hivyo vilivyoingia katika wiki ya 11 sasa.

Soma zaidi:Ukraine: Operesheni ya tatu ya kuwahamisha raia kutoka Mariupol yaaendelea

Zelensky ameorodhesha miji na majijikadhaa ambayo yanadhibitiwa na vikosi vya uvamizi vya urusi akisema katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Ukraine iliwatimua wanajeshi wa Ujerumani ya Wanazi kutoka katika maeneo hayo.

"Majina ya miji hii inatutia moyo leo, yanatupa imani kwamba tutawafukuza walowezi katika ardhi yetu"

Zelensky alisema na kuongeza " Tulishinda wakati huo. Tutashinda na sasa"

Urusi na kumbukumbu ya Siku ya ushindi

Urusi yakanusha kuwalenga raia

Vikosi vya Urusi ambavyo hadi sasa vimedhibiti baadhi ya maeneo muhimu na kushambulia katika makaazi ya raia na majengo ya taasisi ambayo yalitumiwa na raia kama maficho, vimekanusha madai ya Ukraine kuwalenga raia na maeneo muhimu.

katika uvamizi huo ambao Urusi inaita operesheni maalum ya kijeshi, imesababisha idadi kubwa ya raia kulikimbia taifa hilo, huku maelfu wakipoteza maisha kwenye mashambulizi hayo.

Soma zaidi:Putin: "Kama ilivyokuwa 1945, tunashinda"

Hadi sasa majeshi hayo yanaendelea na mashambulizi yakilenga kudhibiti mji wa bandari wa Mariupol.

EU yatarajiwa kutoa majibu ya ombi la Ukraine kuwa mwananchama

Umoja wa Ulaya unatarajiwa kutoa majibu kwa Ukraine mwezi ujao juu ya maombi yake ya kujiunga na uanachama wa umoja huo.

Rais wa Halmashauri Kuu ya umoja huo, Ursula von der Leyen amethibitisha leo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Amesema katika mazungumzo yake na rais Zelensky kwa njia ya simu alimueleza kwamba wapo kwenye hatua muhimu itayotoa muelekeo wa ombi la nchi yake mnamo mwezi June.

Mnamo Aprili, von der Leyen alitembelea Kyiv kuonyesha mshikamano kwa Ukraine na kukubaliana kwamba, Brussels itazingatia azma ya muda mrefu ya Ukraine kujiunga na umoja huo.

Kuidhinishwa kwa Ukraine kama mwanachama wa wa Umoja huo, unasalia katika maamuzi ya nchi wananchama 27, baada ya kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka kwa tume ya von der Leyen, ambayo itasimamia mchakato mgumu na unaoweza kuwa mrefu.

EU yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi vikiwemo vya mafuta