1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Ukraine yasema Urusi inaongeza mashambulizi mji wa Avdiivka

28 Novemba 2023

Vikosi vya Urusi vimezidisha mashambulizi yake vikilenga kuukamata mji wa mashariki wa Ukraine wa Avdiivka, hayo ikiwa ni kulingana na afisa mmoja wa mji huo aliyekaririwa na shirika la habari la Reuters jana Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4ZVYG
Ukraine | Avdiivka | Donetsk
Mapigano ya kuwania mji wa Avdiivka kati ya Urusi na Ukraine yameleta taathira kubwa kwenye mji huo wa viwanda mashariki mwa Ukraine.Picha: Aris Messinis/AFP

Afisa huyo Vitaliy Barabash ambaye kiongozi wa utawala wa kijeshi wa mji huo, amesema wapiganaji wa Urusi wanajaribu kusonga mbele kutoka pande zote baada ya wiki kadhaa za mapigano makali.

Maafisa wa mji huo wanasema hakuna jengo hata moja lililosalimika sehemu kubwa ya wakaazi wamekimbia mji huo wa viwanda kufuatia miezi kadhaa ya mapigano yaliyopamba moto katikati mwa Oktoba.

Urusi imekuwa ikitumia mashambulizi ya anga na vikosi vya ardhini kuwazidi nguvu askari wa Ukraine kwenye mji huo ambao iwapo Moscow itaukamata itakuwa ni pigo kubwa kwa serikali mjini Kyiv.