1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine kupewa hadhi ya kuwania kuingia Umoja wa Ulaya?

Sudi Mnette
23 Juni 2022

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameyaambia mataifa ya Balkani ya Magharibi kuwa kwa sasa yanapaswa kutumia fursa kujiunga na Umoja wa Ulaya, baada ya kuifanyia kazi jitihada hiyo kwa miaka mingi.

https://p.dw.com/p/4D7KT
Belgien Brüssel 2017 | Michel Barnien, Brexit-Unterhändler
Picha: Emmanuel Dunand/AFP/Getty Images

Kabla ya kuanza kwa mkutano wa mataifa ya Umoja wa Ulaya na yale ya Balkani Magharibi, Kansela Scholz aliwaambia waandishi wa habari raia katika eneo la mataifa hayo wamekuwa wakiisubiri fursa hiyo ya kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya kwa karibu mika 20.

Amesema ni muhimu kwamba hatua hiyo ambayo imekuwa ya ahadi ya kuaminika, kwa vile jitihada nyingi ambazo mataifa hayo zimechukua lazima zifikie ukomo na kimsingi zihitimishwe kwa uandikishwaji wao katika umoja huo huku akitoa ahadi ya Ujerumani kusaidia katika kifukiwa kwa lengo hilo.

Ukraine inaweza kuwa mgombea wa nafasi ya kuingia katika Umoja wa Ulaya.

Ukraine | Olaf Scholz und Wolodymyr Selenskyj
Kansela Olaf Scholz na Rais Volodymyr ZelenskyPicha: Sergei Supinsky/AFP/ Getty Images

Katika muendelelezo wa hatua ya mataifa kujiunga na Umoja wa Ulaya, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel amesema viongozi wa umoja huo wanatarajiwa kutoa uamuzi wa kihistoria wa kuipa hadhi ya kuwania nafasi ya kujiunga na umoja wao, Ukraine pamoja na taifa jirani la Moldova.

Nchini Ujerumani Waziri wa Uchumi, Robert Habeck leo hii anatarajiwa kuutangaza mpango wa dharura wa matumizi ya gesi ya taifa kufuatia mzozo unaoendelea wa Urusi. Hatua hiyo ina maana kwamba kuna tatizo katika usambazaji wa gesi au uhitaji wa kiwango cha juu wa kupita kiasi, hali inayozorotesha mchakato wa usambazaji.

Tamko hilo linahusiana na kitendo cha juma lililopita cha Urusi cha kupunguzwa kwa kasi gesi inayoingizwa Ujerumani kwa kupitia bomba la Nord Stream 1, ambayo Mamlaka ya Ujerumani inasema imechochewa kisiasa.

Maeneo ya utamaduni na historia 152 yameshambuliwa Urusi.

Katika hatua nyingine wataalamu wa Umoja wa Mataifa wemetoa uthibitisha wa uharibifu kamili au wa kiasi fulani wa maeneo ya turathi ya dunia na utamaduni takribani 152 nchini Ukraine tangu Urusi ilivamie taifa hilo. Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO limesema uharibufu huo unayahusisha majumba ya makumbusho na makaburi, makanisa na majengo mengine ya kidini.

Soma zaidi:Ukraine yataka Urusi iwekewe vikwazo zaidi

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema kitendo cha kuyashambulia maeneo ya kitemaduni lazima kiachwe. Urithi wa kitamadanuni, kwa namna yoyote ilivyo haupaswi kushambuliwa.

Vyanzo: RTR/AFP/DPA