1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatangaza kikosi cha michuano ya Euro 2024

16 Mei 2024

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani Julian Nagelsmann ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoshiriki michuano ya Euro 2024.

https://p.dw.com/p/4fwq1
Julian Naglesmann
Kocha wa Timu ya Ujerumani Julian NaglesmannPicha: Alexander Hassenstein/Getty Images

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani Julian Nagelsmann ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoshiriki michuano ya Euro 2024.

Ujerumani itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo majira ya joto, imetoa orodha kamili ya wachezaji watakaoiwakilisha.

Wachezaji wenye uzoefu Toni Kroos na Thomas Müller ni miongoni mwa wachezaji waliotajwa katika kikosi cha kocha Nagelsmann.

Michuano ya Kombe la EURO 2024 yakaribia

Hata hivyo, beki katika safu ya ulinzi ya timu ya Borussia Dortmund Mats Hummels, kiungo mkabaji wa Bayern Munich Leon Goretzka na winga Serge Gnabry hawakujumuishwa.

Wengine waliotaja leo ni pamoja na Alexander Nübel, Marc-André ter Stegen, Oliver Baumann,

Jamal Musiala, Waldemar Anton, Benjamin Henrichs na Maximilian Beier. Orodha hii imewataja wachezaji 12 pekee kutoka kwenye kikosi cha wachezaji 26 kilichoshiriki Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.

Hata hivyo kikosi cha mwisho kinapaswa kuwasilishwa ifikapo Juni 7 na hakiwezi kuwa na zaidi ya wachezaji 26.