1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza na Frontex wasaini mkataba wa ushirikiano

Josephat Charo
24 Februari 2024

Mkurugenzi Mkuu wa kikosi cha ulinzi wa mpakani cha Uingereza Phil Douglas na Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa Frontex Hans Leijtens walisaini mkataba huo jijini London.

https://p.dw.com/p/4cpHA
Hans Leijtens
Mkurugenzi wa wakala wa Frontex, Hans LeijtensPicha: Virginia Mayo/AP/picture alliance

Uingereza imesaini mkataba na wakala wa ulinzi wa mpakani wa Umoja wa Ulaya Frontex kuimarisha ushirikiano wa mpakani na kupambana kwa pamoja dhidi ya uhamiaji usio halali.

Serikali ya Uingereza imesema hatua hiyo inanuiwa kudhibiti uhamiaji usio halali kupitia ujia wa English Channel kutoka bara la Ulaya.

Wakala wa Frontex umesema ushirikiano huo umejikita katika maelewano ya pamoja kwamba usimamizi mzuri wa mpaka unahitaji ushirikiano wa karibu katika mipaka.

Makubaliano hayo ni mwanzo wa awamu ya kupanga na maelezo bado hayajawekwa wazi. Frontex imesema pande zote zitashirikiana kwa pamoja kuainisha mipango mahususi ya ushirikiano.