1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waisraeli wazuiwa kujiunga na chuo cha ulinzi Uingereza

15 Septemba 2025

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imetangaza kuwapiga marufuku Waisraeli kujiunga na chuo mashuhuri cha masuala ya ulinzi nchini humo, kufuatia kile kinachojiri kwenye vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/50VbT
London 2025 | Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer Picha: Toby Melville/AFP/Getty Images

Hii inamaanisha kuanzia mwaka ujao wanafunzi kutoka Israel hawatokubaliwa kujiunga na chuo hicho kinachotoa mafunzo ya kimataifa ya kimkakati kwa wanafunzi wa Uingereza na maeneo mengine ya dunia.

Israel imekasirishwa na uamuzi huo iliyouita wa kibaguzi unaokwenda kinyume na tamaduni za Uingereza za uvumilivu, utu na uadilifu.

Ingawa Uingereza inabakia kuwa mshirika wa karibu wa Israel, lakini hivi karibuni imekuwa ikiishinikiza nchi hiyo kuachana na vita vyake huko Gaza, ikitishia mwezi Julai kuitambua Palestina kama dola huru iwapo Israel haitochukua hatua za kupunguza operesheni zake huko.