1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tusk atarajia kutatuwa mgogoro wa Poland na Ukraine

Mohammed Khelef
22 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk amesema serikali yake na ile ya Ukraine zitaweza kutatua masuala tata baina yao, ambayo ni pamoja na machafuko ya hivi karibuni kwenye mpaka baina ya mataifa hayo.

https://p.dw.com/p/4bXzm
Ukraine | Vita | Ziara Donald Tusk mjini Kiew
Waziri Mkuu wa Poland, Donald Tusk (kulia), akikaribishwa na mwenzake wa Ukraine, Denys Shmyhal, mjini Kiev.Picha: Viacheslav Ratynskyi/REUTERS

"Pia tuna masuala mengi ya nchi zetu ya kujadili, ikiwa ni pamoja na maslahi. Kuna baadhi ya migogoro ya kimaslahi, tunajua hili vizuri na tutalizungumzia, lakini katika mtazamo sio tu wa kirafiki, ulio dhahiri, bali pia kwa mtazamo wa kutatua matatizo haya haraka iwezekanavyo, badala ya kuyaendeleza na kuyazidisha." Tusk aliyasema hayo baada ya mazungumzo na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine siku ya Jumatatu (Januari 22) katika ziara ya kiongozi huyo mjini Kyiv.

Rais Zelensky kwa upande wake amethibitisha hilo kwa waandishi wa habari akisema wamejadiliana na Tusk juu ya kusuluhisha masuala yote tete yanayowakabili katika kiwango cha serikali na hatua hilo litaanza hivi karibuni. 

Ukraine na Poland pia zimehitimisha mazungumzo ya uwekezaji katika uzalishaji wa pamoja wa silaha na risasi.