1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Tume ya uchaguzi: Rais Museveni anaongoza kwa asilimia 61.7

16 Januari 2026

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi, yanampa ushindi rais Yoweri Museveni kwa asilimia 61.7 ya kura halali ambazo zimekwisha hesabiwa hadi sasa.

https://p.dw.com/p/56uec
Kampala I Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akihutubia wafuasi wa chama tawala cha NRMPicha: AFP

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa ndani ya saa 48 baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika. Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini  Uganda  baada uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kufanyika hapo jana licha ya kasoro mbalimbali kushuhudiwa.

Lakini tayari mwanasiasa mkuu wa upinzani na anayegombea urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine anaishutumu serikali kwa "wizi wa kura" na kuwakamata baadhi ya maafisa wa chama chake. Baadhi ya kura zimeonekana kuhesabiwa kwa uwazi huku kukiwa hakuna vurugu zozote kubwa zilizoripotiwa.