1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kuomba kubadilishiwa jaji

7 Agosti 2023

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, alisema angeliwasilisha ombi la kutaka kubadilishiwa jaji katika kesi yake ya kihistoria ya jinai na kwamba kesi hiyo ihamishwe kutoka Washington.

https://p.dw.com/p/4UqaS
USA | Donald Trump
Picha: Butch Dill/AP/picture alliance

Trump anayekabiliwa na mashtaka ya kujaribu kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 na kuwalaghai wamarekani, anataka Jaji Tanya Chutkan abadilishwe akisema hawezi kupata hukumu ya haki katika kesi aliyoitaja kuwa ya kipuuzi inayohusu uhuru wa kujieleza na uchaguzi wa haki.

Soma zaidi: Trump akana mashitaka yanayohusiana na uchaguzi

Hata hivyo, wakili wa Trump, John Lauro, amekanusha taarifa hiyo na kusema hakuna uamuzi wowote wa mwisho uliochukuliwa.

Makamu wa rais wa zamani, Mike Pence, ambaye ndiye mhusika mkuu katika kesi hiyo, amesema hatokataa kutoa ushahidi mahakamani.