1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aususia mdahalo wa wanasiasa wa Republican

27 Septemba 2023

Wanasiasa wanaowania kuteuliwa na chama cha Republican kuwania urais nchini Marekani watachuana leo usiku kwenye mdahalo wa pili kiasi miezi minne kabla ya kuanza kwa kura za mchujo wa kumtafuta mshindi.

https://p.dw.com/p/4Wsw6
Mwanasiasa na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Mwanasiasa na rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Sue Ogrocki/AP Photo/picture alliance

Wagombea saba wa chama hicho watapambana kwenye mdahalo huo utakaofanyika huko California na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Fox. 

Hata hivyo, rais wa zamani Donald Trump anayeongoza kura za maoniza kumpata mgombea wa Republican, hatoshiriki mdahalo huo kama ilivyokuwa kwa mchuano wa kwanza uliofanyika mwezi uliopita. 

Soma pia:Mahakama yamtia hatiani Trump kwa udanganyifu

Badala yake anapanga kuwahutubia wafanyakazi wa sekta ya kuunda magari walio kwenye mgomo wa kudai nyongeza ya mishahara.

Miongoni mwa wanaoshirika mdahalo wa leo ni makamu wa zamani wa rais, Mike Pence, na gavana wa jimbo la Florida, Ron DeSantis.