1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump aitisha maandamano kupinga uwezekano wa kumkamata

Zainab Aziz
19 Machi 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amedai kwamba atakamatwa siku ya Jumanne kutokana na kesi iliyofikishwa kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa Manhattan.

https://p.dw.com/p/4OtmG
USA I Donald Trump - NCAA Wrestling Championships
Picha: Sue Ogrocki/AP/picture alliance

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema anatarajia kukamatwa na polisi siku ya Jumanne, katika kesi iliyofikishwa kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa Manhattan Alvin Bragg. Hata hivyo Trump hakutaja tuhuma zitakazosababisha akamatwe. Rais huyo wa zamani wa Marekani ameituhumu kwa rushwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa mji wa Manhattan huku akiwataka wafuasi wake waandamane kupinga hatua hiyo.

Hayo yanajiri wakati Trump amekwishatangaza nia yake ya kugombea urais mwakani. Mapema mwaka huu, Ofisi ya Bragg  ilianza kuwasilisha ushahidi kwa jopo la majaji ili kuchunguza malipo ya dola za kimarekani 130,000 yaliyofanywa na mwanasheria binafsi wa zamani wa Trump Michael Cohen kwenda kwa mcheza filamu za ngono Stormy Daniels katika siku za mwisho za kampeni ya Trump ya mwaka 2016. Hadi sasa hakuna rais wa Marekani ambaye amekabiliwa na mashtaka ya jinai.